Simu zetu zimetokea kurahisisha mambo mengi tuu katika matumizi yetu ya kila siku kiasi kwamba kuna vitu vingine unaona ni shida kutembea navyo kutokana na kwamba rununu uliyonayo inaweza ikafanya kile ambacho ungekifanya kupitia kipakatalishi.
“Hakuna aliyezaliwa anajua” bali sote tulijifunza na tunajifunza. Kama kitu hujawahi kukitumia hata mara moja au ukiwa unakitumia kwa nadra sana (maara chache) kupata changamoto jinsi ya kukitumia ni jambo la kawaida kwani kuna msemo wa Kiingereza unasema “Practice makes perfect” kwa maana ya kwamba unapofanya jambo mara kwa mara ndio unalifanya kwa ufasaha zaidi.
Mimi ni mmoja kati ya wale watu ambao wanatumia sana mawasiliano kwa njia ya barua pepe kuliko hata WhatsApp, Telegram, n.k. Basi kwa sababu nilikuwa nataka kuambatanisha kitu kiende pamoja na ujumbe nikajikuta napata shida kuweza kuweka kitu hicho kupitia simu aina ya iPhone. Hapo ndio ilinibidi niwaze namna gani nitweza kufanikisha adhma yangu na hatimae kuwa mwalimu kwa wengine. Baada ya kufahamu nilicheka sana kutokana na ukweli kwamba ilikuwa ni kitu kidogo sana ambacho kilitakiwa kifanyike ili kukamilisha zoezi zima.
Fuata njia hizi ili kuweza kuambatanisha kitu ndani ya ujumbe wa barua pepe kwenye iPhone/iPad.
Kwenye uwanja wa kuandika ujumbe huku utambulisho wako ukiwa ni barua pepe, programu tumishi ikiwa ni Mail lakini pia ukiwa unafanya zoezi hilo kupitia iPhone au iPad basi fuata njia zifuatazo na nina hakika utafnikiwa:-
Njia ni moja na rahisi sana wewe bofya mara mbili (2) kwenye ile sehemu ya kuandika ujumbe (chini ya kipegele cha subject) halafu unaona menyu inatokea ikiwa ina vipengele vya “Select“, “Select all“, “Quote level“, halikadhalika na mshale wa kwenda kulia, wewe bonyeza huo mshale kisha nenda moja kwa moja palipoandikwa “Add Attachment“; ndio kipengele kitakachokuwezesha kuambatanisha kitu kwenye uwanja wa ujumbe wa maandishi.
Sasa kwa kuhitimisha niseme tuu tujifunze kuwa mwepesi kutumia barua pepe kama mojawapo ya njia kumfikishia mhusika ujumbe na hatimae tutaweza kujifunza kila mara kuliko kutegemea WhatsApp.
Vyanzo: Mawazo binafsi, Tech Greatest
0 Maoni