Ngoja kwanza, ngoja kwanza!…..hivi unajua BongoTech soon itapatikana katika App ya Telegram? tuendelee sasa, iOS13 iko mbioni kutoka, mengi ya kuvutia yapo lakini leo tuguse tuu kwenye kipengele kimojawapo.
Swala la chaja kuisha katika kifaa cha Apple ni swala la kawaida sana hawa ukiwa umewasha data (intaneti). jambo ambalo liko wazi ni kwamba betri za simu janja kadri siku zinavyokwenda huwa zinapungua ubora wake, kwa mfano simu yako ikijaa asimilia 100 ikiwa mpya na ikifikisha mwaka uwezo wa chaja kuisha lazima utakuwa ni tofauti.
Apple wameliona hilo na wao wamesema kuwa simu za iPhone zinapata adha hiyo mara nyingi endapo zitaachwa katika chaja ingali ya kuwa zimefikisha asilimia 100 za ujazo wa chaji. Jambo hili mara nyingi huwa linatokea usiku sio? simu zetu tunaziacha huku zikiwa zinajaa chaji usiku kucha.
Hii inamaanisha kuwa kuiacha kwa kipendi kierefu kidogo angali ya kuwa imejaa kwa asilimia mia. Sasa ili kuepuka na sekeseke hilo iOS13 itakua na kipengele mahususi kwa ajili ya betri ambacho kinaitwa ‘Optimised Battery Charging’. kipengele hiki ni mahususi kwa kupunguza maisha ya betri yako (kupunguza muda wa kuchoka)
Kupunguzwa huko kwa muda wa kuchoka kunafanyika katika hali ya kwamba kinapunguza muda ambao iPhone yako inautumia ikishakuwa imejaa kabisa asilimia 100.
Kwa kifupi ni kwamba simu yako kwa kutumia teknolojia hii basi itaweza kukusoma tabia zako za kuchaji simu katika hali ya kwamba simu itafanya mikakati na mipango ya kuchaji betri la simu hiyo. kwa mfano inaweza ikachaji betri mpaka asilimia 80 usiku kwa haraka kabisa na hizo 20% zilizobaki ikazimalizia asubuhi wakati unakaribia kuamka.
Ubaya wa kipengele hiki ni kwamba unaweza ukashangaa simu yako isiwe imejaa kabisa kama ukiwahi kaumka, lakini kwa upande mwingine hii ni nzuri kwani una uwezo wa kuwasha na kuzima kipengele hiki….. kama unajali maisha ya betri ya simu yako… maamuzi ni yako
Ningependa kusikia kutoka kwako, kipengele hiki kitaanza onekana ramsi katika toleo la iOS13 ambalo linanatoka mwezi wa 9 mwaka 2019, niadikie hapo chini sehemu ya comment hili unalionaje? je kipengele kina umuhimu au ni cha kawaida sana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa BongoTech Kila Siku Kwa Habari Za Sayansi Na Teknolojia Kwa Ujumla. Kumbuka BongoTech Daima Tupo Na wewe Katika Teknolojia!.
Usisahau Telegram
0 Maoni