Inafahamika wazi kuwa simu za Android kama vile Samsung Galaxy ndio wapinzani wakubwa wa kampuni Ya Apple ambao wana iPhone zinazotumia iOs. Watu wengi wanasema simu za android ni rahisi kutumia kuliko zile za Apple, Mimi nasema inategemea na mtu na chaguo lake (ha!). Watumiaji wa Android wanafurahia maelfu kwa maelfu ya aplikesheni (Application) zinazopatikana bure Google play.
Lakini kushusha aplikesheni nyingi katika simu yako inashusha kasi ya ufanyaji kazi wa simu yako, Je hili likitokea unafanyaje?. ikitokea hivi ni vizuri kureset simu yako, Lakini pia kureset simu yako kuna kanuni zake na zisipofuatwa unaweza jikuta unaharibu kifaa (simu) chako. Twende wote sambamba kuzijua njia tatu za kureset simu au tableti yako ya Android
Jinsi Ya Kureset Simu/Tableti Ya Android
Kabla ya kufuata maelezo haya kureset kutafuta Data zako zote zilizo kwenye simu (number za simu,miziki,picha,notes,mafile ulioshusha kutoka GooglePlay n.k). Hivyo basi unashauriwa kufanya back up ya data zako kwanza. Kisha Toa laini na Memori Kadi katika simu Hiyo ya Android Pia inashauriwa charge iwe angalau asilimia hamsini (50%).
1. Kureset Kwa Kutumia Factory Reset
Hi ni njia rahisi kabisa ya kureset simu yako. kinachotakiwa ni kwenda kwenye Menu ya simu yako kisha unaenda kwenye Settings kisha unabofya Backup And Restore baada ya hapo unaenda kwenye Factory Reset. Kitu cha muhimu kujua hapa ni kwamba ukifanya hivi vitu vyako vitafutika hivyo ni muhimu kufanya back up ya data zako zote kabla hujafanya hivi.
kuna baadhi ya simu facory reset haipatikani kama ilivyoelekezwa hapo juu, nenda kwenye Privacy Settings
2. Kureset Kwa Kutumia USSD kodi
Watengenezaji wa simu wengi kama Samsung, HTC n.k huwa wanatoa kodi inayoweza ku ‘restore’ simu ya Android. Kodi hiyo ni *#7780# kwa hiyo kila utakapo piga hiyo kodi simu yako ya adroid itakuuliza kufomati. Ni vizuri kuback up data zako pia kwa sababu baadhi ya simu haziulizi ukipiga tuu hiyo kodi simu inaanza kufomati
3. Kureset Kwa Kutumia System Restore
Hi njia ya mwisho ni ngumu kidogo na haifahamiki sana laki ndio njia yenye nguvu kuliko hizo mbili hapo juu. Sifa za njia hii ni kwamba inafanya kazi hata simu yako ikiwa imeji ‘lock’ (kama umesahau pattern au password ya simu yako). Njia (1 na 2) hazitafanya kazi kama simu yako itakua imeji ‘loki’
JINSI
A. Zima Simu Yako Ya Android
- Kama ni Mtumiaji Wa Samsung Bonyeza: Sauti juu + Home + Kuzima. Mara baada ya simu kunguruma achia kitufe cha kuzima. Mara simu ikiwa katika modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha sauti juu na cha home pia
- Kama Ni Mtumiaji Wa HTC Bonyeza: Sauti Chini + Kuzima. Simu ikiwa inawaka achia kitufe cha kuwasha, ukiona imetokea modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha Sauti Chini
- Kama Ni Mtumiaji Wa Micromax Bonyeza: Sauti Juu + Kuzima
B. Ukishaingia katika menyu ya System Restore tumia kitufe cha Sauti Juu Na Sauti Chini Kuchagua chaguo lako na kitufe cha kuwasha/kuzima simu kuchagua chaguo hilo
C. Sasa chagua chaguo lako kureset simu yako ya Android
Hii njia itachukua mda kidogo katika ufanyaji kazi wake laki unashauriwa kutotoa betri ya simu yako maana italeta hitilafu wakati wa kureset . Naimani njia hizi tatu zitakusaidia sana kureset simu yako mwenyewe bila kuwapelekea mafundi au wataalamu wowote maana utaingia gharama. Kwa nini ulipie kazi ambayo unaweza ifanya mwenyewe?
Ningependa kusikia kutoka kwako, Simu yako iko Slow?, imeji Lock?, Hizi njia umezijaribu? Zimetatua matatizo yako?
0 Maoni