Vitu vipya kwenye WhatsApp safari hii
WhatsApp wamekuwa wakiboresha (kuweka vitu vipya) programu tumishi hiyo ambayo kila leo haichoshi kuitumia na kwa wengine kuwa njia rahisi sana ya kufanya mawasiliano kwa haraka zaidi.
Unatakata kupakua app za whatsapp : Bonyeza hapa
Katika kuzidi kuendelea kuvutia watumiaji wa WhatsApp kuna mambo kadha wa kadha ambapo toleo la programu tumishi linalowekwa masasisho kabla ya watumiaji wengine watakuwa wameshakutana na mambo haya ambayo naenda kuyazungumzia lakini iwapo tu wanatumia toleo la karibuni kabisa.
>Kupitia kitu kabla ya kukisambaza.
Katika masasisho ambayo yanapatikana toleo la majaribio namba 2.18.325 (kwa wanaotumia simu za Android) wamekutana na mabadiliko kidogo pale wanapotaka kutumia kitu kwa watu wengi; ukishabonyeza kitufe cha kutaka kusambaza kuna menyu ndogo inatokea mara moja ambayo inakupa uwanja wa kufikiria kwa mara ya pili iwapo unataka kuongeza, kupunguza ama kuachana kabisa na huo mpango.
>Kumjibu mtu katika faragha.
Bado suala zima la usiri ni kivutio kwani hivi sasa wanaotumia WhatsApp Beta toleo namba 2.18.355 watakuwa wameona kipengele kipya cha “Reply privately” kwenye kundi na kwa tafsiri isiyo rasmi maana yake ni kumjibu mtu katika faragha bila ya watu wengine kujua kuwa aliyetuma ujumbe fulani ameshajibiwa.
Uktaka kupata kipengele hicho kipya kwenye kikundi basi bofya kwa sekunde moja ujumbe mhusika unayetaka kumjibu kisha bofya kwenye zile nukta tatu na menyu ndogo itatokea ambapo utachagua “Reply privately“.
>Kuwa mapumzikoni kupokea jumbe.
Unaweza ukawa ni mtu ambae unapokea jumbe nyingi kwenye WhatsAp ndani ya muda mfupi lakini kwa maboresho ya hivi karibuni inawezekana kuzuia usipokee vitu kwenye WhatsApp kwa muda fulani utakaopenda wewe mwenyewe, kwa Kiingereza wameita “Vacation mode“.
>Mengineyo.
WhatsApp inaweka vikatuni mbalimbali vipya kwenye programu tumishi husika sasa kitu ambacho kimeongezwa ni uwezo wa kutafuta kikatuni husika ambacho utataka kukitumia kutokana na kwamba vipo vingi.
0 Maoni