Gharama za mawasiliano ni nafuu lakini zinakuwa ni rahisi zaidi iwapo unakuwa unatumia kadi ya simu iliyounganishwa kupata huduma za kipekee (tofauti na nyningine) au kwa lugha iliyozoeleka “Laini za chuo” ambazo huwa zinakuwa zina vifurushi vinavyolenga kumrahishia mawasiliano huyu anayeitumia lakini hasa mwanafunzi.
Mimi ni mtu ambae napenda watu waweze kupata huduma bila ya kwenda mahali husika kufanikisha jambo fulani ninafurahi sana pale ninapoona na kujidhihirishia kuwa mhusika anaweza akajihudumia mwenyewe. Pengine utasema kuwa nimewapaisha wahusika mara baada ya kumaliza kusoma makala hii lakini la hasha! Kitu kizuri ni muhimu kukisifia. Sasa basi pata kufahamu ni nani huyu ninayemzungumzia siku ya leo.
Katika kuperuzi huku na kule nikakutana na kitu kilichonivutia sana nikasema si vibaya nikawashirikisha na wasomaji wangu. Vodacom Tanzania kupitia tovuti yao wana sehemu ambayo mwanafunzi wa chuo anaweza akaomba kupata huduma zinazopatikana kwenye kadi za simu zilizo chini ya “Mwamvuli wa chuo”; hii ikimaanisha kuwa mara baada ya wahusika kupitia ombi lako laini husika itabadilishwa na kuweza kupata ofa za chuo.
Sababu ya kwanini nimevutiwa sana na kitu hicho ambacho Vodacom Tanzania wamekifanya tovuti yao nimeshaeleza lakini kwa kwenda mbali kidogo ni ule uhuru na kuokoa muda kuweza kujisajili wewe mwenyewe huku ukiwa unafahamu kabisa vigezo vinavyohitajika unavyo lakini pia mfumo huu unapunguza sana suala zima la UDANGANYIFU; kujidai kuwa upo kwenye kundi husika lakini kumbe si mwanafunzi wa chuo wala taasisi yoyote ya elimu nchini Tanzania.
Ulimwengu wa kidijiti unazidi kupanuka kila siku na tulipotoka ni tofauti kabisa na hali ilivyo hivi sasa, kumtegemea mtu ndio aweze kukuunganisha na huduma za chuo ni jambo linalopungua polepole. Tembelea KIUNGANISHI HIKI kuweza kujisajili kwa ajili ya kupata ofa za mwanachuo kwa wale wateja wa Vodacom Tanzania.
Chanzo: Vodacom Tanzania
0 Maoni