Notisave: Njia ya kudownload Status za WhatsApp kwa urahisi! #SIMU #MAUJANJA
Notisave ni app ambayo ina uwezo wa kufanya mambo mengi, lakini moja ya kitu muhimu sana unachoweza kuitumia app hii kufanikisha ni kuweza kudownload na kuhifadhi (save) WhatsApp Status za mtu yeyote bila yeye kufahamu.
Notisave ni app inayokuwezesha kupunguza idadi ya taarifa fupi (notifications) zinazotokea kwenye eneo la juu la simu yako, app hii inakuwa sehemu kuu ya wewe kuona notifications zote za apps mbalimbali.

App ya Notisave nje ya kukuwezesha kudownload status za WhatsApp ni app inayokusaidia kuwa na sehemu moja ya kusoma notifications ya app zote za kwenye simu yako kwa mpangilio mwepesi
Kupitia eneo la Chats la app hii utaweza kuona mjumuhisho wa taarifa fupi mbalimbali kutoka apps za kuchati kama vile WhatsApp na Messenger. Kwa upande wa WhatsApp ni eneo hili ndilo utakuta status zote zinazoonekana kwa sasa kwenye app ya WhatsApp.

0 Maoni